Thursday, September 18, 2014
Mwenyekiyi wa Chadema anakaribia Makao Makuu ya Polisi
Mwenyekiyi wa Chadema anakaribia Makao Makuu ya Polisi muda mfupi atakuwa anaingia hapo. Police wameanza kukamata watu waliojitokeza kumsindikiza Mwenyekiti. Huku waandamanaji wanapambana na askari wa FFU vikali. Mji mzima ni balaa. .Tutataheshimiana tu
Majambazi wampora kadinali Brazil
Watu waliokuwa wamejihami wamemuibia Askofu mkuu wa Rio de Janeiro nchini Brazil msalaba wake na pete
Kadinali, Dom Orani Tempesta, alikuwa njiani kuelekea kuhudhuria mkutano mjini alipovamiwa na majambazi hao.
Mmoja wa majambazi aliyekuwa na bunduki katika kanisa, alimfahamu kadinali huyo na kumuomba msamaha.
Hata hivyo, hilo halikushutua genge hilo ambalo liliendleea kumpora kadinali huyo, na hata nusura wampore gari lake.
Vitu vilivyoibwa vilipatikana baadaye.
Hakuna aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo, ambalo lilifanyiika Jumatatu jioni katika mtaa wa Santa Teresa.
Mwandishi wa BBC Gary Duffy, anasema kuwa visa vya wizi hutokea mara kwa mara katika mtaa huo wenye shughuli nyingi za kitalii na kwamba visa hivyo vimekuwa vikiongezeka sana mwaka huu.
Mwanafunzi wa dini pamoja na mpiga picha mmoja waliokuwa kwenye gari na kadinali huyo pia waliporwa.
Licha ya tukio hilo, kadinali aliendelea na shughuli zake huku mwanafunzi na mpiga picha wakienda kuripoti kwa polisi.
Pete ya kadinali na msalaba, vilipatikana pamoja na simu yake ya mkononi
Hata hivyo, vifaa vya mpiga picha havijapatikana.
Dom Orani Tempesta alitawazwa kama kadinali na Papa Francis mapema mwaka huu.
Wandishi wa BBC washambuliwa Urusi
BBC imewasilisha malalamiko kwa serikali ya Urusi baada ya wandishi wake wa habari kushambuliwa Kusini mwa nchi hiyo.
Wandishi hao walikuwa nchini Urusi kuchunguza madai ya baadhi ya maafisa wa usalama wa Urusi kuuawa karibu na mpaka na Ukraine.
Baada ya kuwaarifu maafisa wa huduma ya dharura , waandishi hao walipelekwa katika kituo cha polisi na kuhojiwa kwa saa nne.
Picha walizokuwa wamenasa kwenye kamera zilifutwa wakati wakiwa kwenye kituo cha polisi.
BBC inasema kuwa imechukizwa na kitendo hicho na kutoa wito kwa maafisa wa utawala nchini humo kuchunguza taarifa hizo pamoja na kuwataka kulaani kitendo hicho.
Wednesday, September 17, 2014
Bundi azua tafrani Manzese Dar es salaam
Ndege aina ya Bundi ambaye ni nadra kuonekana nyakati za mchana amezua tafrani na mshangao kwa wakazi wa Manzese big brother baada ya ndege huyo kutua katika moja ya kituo cha kuuza mafuta na kusababisha huduma kusimama katika kituo hicho kwa muda baada ya kundi la watu kujitokeza kwa lengo la kutaka kumshuhudia Bundi huyo.
Bwana Maita Mwana akijitokeza gafla akiwa anakimbia akadai kuwa Bundi yule ni mali yake na ametoroka nyumbani ambako yeye huwa anamfuga
Trafiki aliyegongwa na gari afariki dunia
Trafiki aliyegongwa na gari afariki dunia
Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kituo cha Mbagala, Koplo Riziki Mohamedi ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi) alifariki dunia jana saa 4 asubuhi alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Askari huyo aligongwa juzi asubuhi eneo la Mbagala Rangitatu akiwa anaongoza magari, ghafla gari aina ya Toyota Hiace inayofanya safari zake kati ya Temeke na Kongowe, lilishindwa kushika breki na kumgonga.
Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya fahamu, Moi, Patric Mvungi alithibitisha kufariki kwa askari huyo. “Huyu askari alilazwa Moi tangu jana (juzi) na amefariki leo (jana) saa 4 asubuhi,” alisema Mvungi.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kienya Kienya, alisema utaratibu wa mazishi unafanywa.“Tuko kwenye majonzi na tunafanya maandalizi ya maziko, kwa sasa tunawasiliana na ndugu wa marehemu ili kujua atazikwa wapi na siku gani hivyo utaratibu ukikamilika tutawajulisha,” alisema Kienya.
Kienya alisema dereva wa gari lililomgonga askari huyo, liliyagonga magari mengine manne yaliyokuwa mbele yake na kusababisha watu sita kujeruhiwa.“Majeruhi hao walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Aliyeumia zaidi ni huyu askari,” alisema Kienya.
Alisema Polisi wanaendelea kumsaka dereva huyo ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria, kwani alikimbia baada ya ajali kutokea
Monday, September 15, 2014
OCS afumaniwa na mwanafunzi wa Kidato cha Nne
Mkuu wa kituo cha polisi cha Nyamboge kata ya Katoma wilayani Geita akutwa jana chumbani akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha 4.
Wananchi walimteka na kumpeleka kituo cha polisi,mkuu huyo wa kituo cha polisi anadaiwa kwamba siku 10 zilizopita alimuweka mahabusu mwanafunzi huyo kumtisha akubali kufanya nae mapenzi.
Tayari mkuu wa polisi wa wilaya ya Geita amekwenda jana kwenye eneo la tukio.
Mkosamali apata ajali mbaya Bahi mkoani Dodoma
Mkosamali apata ajali mbaya Bahi mkoani Dodoma
Mbunge wa Muhambwe kupitia NCCR-MAGEUZO Felix Mkosamali amepata ajali mbaya ya barabarani eneo la wilaya ya BAHI mkoani Dodoma akiwa njiani kutokea Dodoma kwenda Kigoma.
Yeye Mwenyewe hakuumia sana ila mdogo wake pamoja na abiria mwingine wameumia vibaya na kwa sasa wapo Hospital ya rufaa ya mkoa wa Dodoma wakiendelea na matibabu.
Mungu awaponye mapema Amen.
Askari usalama barabarani afyekwa Na daladala-Mbagala
Hivi punde kuna taarifa za kufyekwa kwa askari Wa Usalama barabarani huko Mbagala akiwa katika jitihada za kulisimamisha dakadala hilo lenye safari za kutoka Temeke kwenda Mbagala chalambe. Askari walikuwa wanne , jitihada za kunasua abiria wanne wengine waliokuwa ndani zinaendelea.
Friday, September 12, 2014
Breaking News: Ajali mbaya Mbezi kwa msuguri!!
Kuna ajali mbaya imetokea hapa Mbezi kwa msuguri ikihusisha Lori LA mchanga na Gari aina ya Toyota Spacio.
Gari. ndogo imeharibiwa vibaya sidhani kama kuna aliyesalimika.
Picha zinatisha sana siwezi kuzianika hapa
Mwanaume na hisia za ujauzito
Harry Ashby ni mwanaume wa kwanza mjini Birmingham kupata ruhusa ya kupumzika nyumbani baada ya kusumbuliwa na homa mithili ya mwanamke mja mzito.
Amekuwa akipatwa na homa za vipindi hasa nyakati za asubuhi baada ya mchumba wake aitwae Charlotte kuwa mjamzito, mtandao wa Itv news umeeleza.
Habari zinasema mwanaume huyo mwenye miaka 29 anayefanya kazi ya ulinzi ,amesema ameongezeka uzito na tumbo limekua mithili ya aliye mjamzito na kudai kuwa anasumbuliwa na maumivu ya mgongo na cha ajabu amekuwa na hamu ya baadhi ya vyakula.
Harry ameripotiwa kuwa na dalili za kuwa mja mzito miezi miwili baada ya kubaini kuwa mchumba wake ni mjamzito.
Harry amekuwa akipatiwa dawa na inasemekana anaweza kudai mafao wakati akiwa katika mapumziko hayo.
Muingereza aliyepona Ebola kurejea Afrika
Mwanaume wa kwanza muingereza kuambukizwa homa kali ya Ebola, katika mlipuko wa ugonjwa huo unaoshuhudiwa katika kanda ya Afrika Magharibi, anatarajiwa kurejea Afrika ambako aliambukizwa.
Anasema anafanya hivyo ili aweze kuwasaidia wengine walioathirika kuweza kupambana na ugonjwa huo ambao ni janga kubwa
William Pooley alipokea matibabu mjini London baada ya kupelekwa nchini humo kutoka Sierra Leone.
Ameweza kupona na hata kuodnoka hospitalini. Lakini kwa sasa anajiandaa kusafiri kurejea Afrika katika wiki chache zijazo.
Pooley mwenye umri wa miaka 29, alisema ana hamu kubwa sana kurejea Afrika na kwamba huenda asiweze kuambikizwa.
Wakati Pooley alipoambukizwa, alikuwa anafanya kazi ya kujitolea nchini Sierra Leone, ambayo ni moja ya nchi za kanda ya Afrika Magharibi zilizoathriwa na ugonjwa huo.
Takribna nusu ya watu 3,000 waliombaukizwa homa hiyo, katika mlipuko wa sasa barani Afrika, ambao ilianzia nchini Guinea, wamefariki.
''Nina hamu sana kurejea kufanya kazi inayonisubiri,'' Pooley aliambia BBC.
"nahisi kama zijaimaliza kazi yangu kwani niliondoka huko mapema sana. Na ninajua kuna kazi nyingi katika nchi hizo, na tunahitaji kuwa huko kuwasaidia watu. ''
Mfungwa apatikana na simu mwilini Kenya
Kwa baadhi ya watu simu ya mkononi ni kifaa tu cha mawasIliano ilihali kwa wengine ni kifa ambacho kinaweza kukuweka katika hali ya kufa kupona.
Mfungwa mmoja nchini Kenya amewaacha wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za mkononi kutolewa mwilini mwake. Inaarifia aliziingiza simu hizo mwilini mwake kupitia sehemu yake nyeti ya nyuma.
Mfungwa huyo wa gereza la King'ong'o katika jimbo la Nyeri alifanyiwa upasuaji Jumanne kutolewa simu hizo ambazo alikuwa amezificha mwilini mwake kupitia sehemu yake ya nyuma.
Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ni kero kubwa kwa maafisa wakuu wa magereza.
Wamekuwa kwa miaka mingi wakijaribu kulikomesha tatizo hilo bila mafanikio.Kwa njia yoyote ile wafungwa huingiza bidhaa kama simu katika magereza nchini Kenya kinyume na sheria za magereza.
Maafisa wa magereza wanakiri kwamba wafungwa hawa wakati mwingine hushirikiana na walinzi wa magereza kuingiza bidhaa katika magereza kimagendo.
Oscar hatiani kwa kuua bila kukusudia
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp pasi na kukusudia.
Akitoa uamuzi wake jaji Thokozile Masipa alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango wake wa choo akiwa akatika hali ya mshtuko akidhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Alisema kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alinuia kumuua Steenkamp na kwamba alifanya mauaji hayo kwa kusudi.
Pia alipatikana na hatia ya kosa la kutumia silaha yake visivyo alipokwenda mgahawani.
Jaji Thokozile Masipa amesogeza muda wa mwanaridha huyo yuko huru kwa dhamana.
Pistorius atakuwa huru hadi hukumu itakapotolewa mwezi ujao, ambapo anaweza kuhukumiwa hadi miaka 15 gerezani. Oscar Pistorius ataendelea kukaa kwa mjombake alikokuwa muda wote kesi ilipokuwa ikiendelea.
Mjombake Pistorius, Arnold Pistorius amemshukuru Jaji Masipa kwa uamuzi wake wa kumuachia kwa dhamana.
Wafanyakazi wa TIGO Mlimani City Wamegoma, mgomo umesababisha ofisi za Tigo mlimani city kufungwa
Habari zilizonifikia hivi punde ni kuwa ofisi za TIGO Mlimani city zimefungwa kutokana na wafanyakazi wa ofisi hizo, kucheleweshewa mshahara wao, watu wamejazana nje.
Wafanyakazi hao wa TIGO wamekataa kufanya kazi mpaka watakapo lipwa mishahara yao.
Lawama zinawaendea kampuni ya NFT kuwa wao ndo hawajatoa hela, hivyo kusababisha huduma kufungwa.
Habari zinasema hii kampuni ya NFT ina kawaida ya kuwacheleweshea mishahara wafanyakazi wao, wanatoa mishahara wanapojisikia.
Jaji Warioba: Bunge lisitishwe
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema ni vyema Bunge Maalumu la Katiba likasitishwa kwani Katiba bora haiwezi kupatikana kwa muda wa wiki mbili.
Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja siku moja baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kumtaka Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, kulisitisha, huku mwenyewe akisema litaendelea na hadi kufikia Oktoba 4 Katiba inayopendekezwa itapatikana.
Jaji Warioba alieleza kushangazwa kwa haraka waliyokuwanayo wajumbe wa Bunge hilo wakati wanajua kuwa Katiba haiwezi kupatikana kwa muda uliobaki.
Alisema wiki mbili au tatu zilizobaki ni chache mno na kwamba Katiba mpya haiwezi kupatikana, hivyo ni vyema sasa busara ikatumika kulisitisha.
“Mimi sizungumzii kauli ya Ukawa, lakini natoa maoni yangu kwamba sidhani kama watamaliza kwa kipindi hiki kifupi, kuna mambo hawawezi kupata kwa muda huu mfupi.
“Ninachotaka watumie tu busara waliahirishe… sijui haraka yao hii ni ya nini. Kwanini wanashindwa kuelewa kuwa Katiba ni suala la maridhiano?” alihoji Jaji Warioba.
Kwa upande wake, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Augustino Ramadhani, alikataa kuzungumzia chochote juu ya suala hilo, akisema tangu Rais Jakaya Kikwete alizindue Bunge hilo, alijitoa kuzungumzia suala la Katiba.
“Kama umefuatilia nilishajitoa tangu siku Rais Kikwete anazindua Bunge la Katiba, nilijitoa kabisa, sitaki kabisa kuzungumzia Katiba tena,” alisema Jaji Ramadhani.
Alipotakiwa kueleza sababu za yeye kujitoa kuzungumzia Katiba, alisema: “Ni uamuzi wangu.”
CHEYO NA UKAWA
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), John Cheyo, alisema Bunge hilo haliwezi kusitishwa wala kuongozwa kwa matakwa ya watu waliopo barabarani.
Akizungumza wakati akichangia majadiliano ya jumla ya mchakato wa Katiba mpya, alisema makubaliano yaliyofikiwa baina ya TCD na Rais Kikwete, ni kuhakikisha Bunge hilo linapata Katiba mpya iliyopendekezwa na wananchi.
Cheyo alisema kuwa Bunge hilo linaendelea na kazi yake kwa mujibu wa sheria.
Alisema maandamano yanayotarajiwa kufanywa na vijana wa vyama vinavyounda Ukawa, hayatasaidia lolote.
Alielezwa kushangazwa kwake na matamko ya Ukawa na kueleza kuwa ukweli wa kile kilichojadiliwa upo kwenye video ambayo inaonyesha kila mmoja alivyochangia majadiliano hayo.
“Katiba itakayodumu ni ile ya maridhiano, lakini katika maridhiano haina maana kwamba wanaokaa kuzungumza lazima wang’ang’anie upande wao.
“Wanaokaa kuzungumza maana yake wanatafuta ni vitu gani ambavyo wanaweza kuvizungumza, na ni vitu gani ambavyo vinaweza hata kuwekwa pembeni kwa sasa, lakini baadaye vikaja kushughulikiwa kwa mazingira ya wakati huo, hili tumejifunza tulipokuwa tunazungumza na Mheshimiwa Rais juu ya mchakato wa Katiba na Uchaguzi Mkuu wa 2015.
“Mheshimiwa Rais amekuwa ni mfano mzuri wa kukubali kushauriana, na kama Katiba tunavyoizungumza hapaswi hata kukubali, lakini amejiweka chini akakaa kitako na viongozi wa TCD na viongozi wanaojiita Ukawa,” alisema Cheyo.
Aliongeza kuwa katika mkutano wa kwanza uliochukua muda wa saa nne, majadiliano yalikuwa ni namna gani Katiba itapatikana na Uchaguzi Mkuu utafanyikaje na si vinginevyo.
Moja ya mambo yaliyokubalika ni Bunge la Katiba lipate Katiba inayopendekezwa na wananchi kama ilivyokusudiwa.
“Pia tulikubaliana kwa hali halisi ya muda tulionao haiwezekani mchakato mzima ukamalizika, na maana ya kumalizika mchakato ni kura ya maoni ya wananchi na ndio wenye Katiba,” alisema.
Cheyo alisema katika makubaliano hayo, viongozi wote waliafikiana kuwa awamu ya Bunge Maalumu imalize kazi yake kama ilivyokuwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
“Bunge hili haliendeshwi kwa amri ya mtu aliyepo barabarani, linaendeshwa kwa mujibu wa sheria ambayo inasema uhai wa Bunge ni Oktoba 4, mwaka huu, wote tulikubaliana,” alisisitiza Cheyo.
Alisema si rahisi Rais akurupuke na kuliahirisha Bunge hilo kwa shinikizo lolote kwa sababu sheria imeweka wazi ukomo wake.
Aliwataka viongozi wa Ukawa kukubaliana na tamko alilolitoa mbele ya vyombo vya habari, ambalo lilipatikana baada ya makubaliano.
Aidha aliwataka wajumbe wenzake kujiamini na kwamba ripoti itakayotolewa na Kamati ya Uandishi ndiyo itakuwa Katiba inayopendekezwa.
“Na kwa sababu yoyote ile, huko nje kuna anayeamini vingine, anaweza kuamini Serikali tatu, na haipo, mimi sitaki, anaamini Kadhi na haipo hiyo ni shauri yako…,” alisema Cheyo.
TEC YAWASHANGAA UKAWA
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severine Niwemugizi, alisema Ukawa walikuwa na kikao cha maridhiano na Rais Kikwete, hivyo walikuwa na nafasi ya kumtaka asitishe Bunge.
Alisema badala yake walitoka kwenye kikao hicho na kuanza kulalamikia wananchi huku wakiwaambia waandamane ikiwa Rais Kikwete atashindwa kusitisha shughuli hizo.
“Inashangaza kuona Ukawa wanalalamika nje ya kikao wakati walikuwa na nafasi kubwa ya kumwambia Rais Kikwete asitishe Bunge mara baada ya kumalizika kwa kikao chao, badala yake wameamua kuja kwa wananchi na kuanza kulalamika.
“Kwani katika hicho kikao hawakuwa na makubaliano? Na kama ni hivyo kwanini walikubali kutumia Katiba ya mwaka 1977 kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani?” alihoji.
Alisema katika kikao hicho Ukawa na Rais Kikwete waliingia makubaliano ya kusitisha mchakato wa Bunge hadi mwaka 2016 ikiwa Rais ajaye atakubali kuendelea nao.
“Nimewashangaa sana wajumbe wa Ukawa, kwa sababu walikuwa na nafasi kubwa ya kuwasilisha malalamiko yao kwa Rais na kuingia makubaliano ya kusitishwa kwa shughuli hizo, lakini baada ya hapo wanakuja kwa wananchi na kuanza kulalamika huku wakidai kuitisha maandamano, kwani hawakuwa na nafasi ya kumwambia rais malalamiko yao,” alisema.
MBOWE
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, alisema hakuna sababu ya kuharakisha mchakato huo na kuwa hata ikibidi baada ya miaka 100, Katiba bora itapatikana.
Alisema jambo muhimu ni Katiba kukidhi mahitaji ya Watanzania na izingatie maoni yao.
“Hatuwezi kuvumilia kuona uchakachuaji wa fedha, unyanyasaji, na ukatili. Yanayoendelea kwenye Bunge la Katiba ni unyama na wizi,” alisema Mbowe.
Thursday, September 11, 2014
Mahakama:Pistorius hakukusudia kuua
Jaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius, amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Hata hivyo jaji huyo Thokozile Masipa amepinga ushahidi wa upande wa utetezi kwamba mwanariadha huyo hakunuia kutenda uhalifu alipomuua mpenzi wake Reeva.
Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana lakini amekana kumuua kwa maksudi , akisema alidhani kuwa mwizi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mshitaka unasisitiza kuwa Pistorius alimuua Reeva kwa maksudi,baada ya wapenzi hao wawili kutofautiana.
Mandishi wa BBC anasema kuwa jaji Thokozile Masipa heunda akachukua hadi Ijumaa kumaliza uamuzi wake.
Pia atakuwa anaangalia kwa makini ukweli wa mashahidi waliotoa ushaidi wao katika kesi hiyo akiwemo Pistorius mwenyewe.
Pistorius huenda akafungwa jela miaka 25 ikiwa atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake.
Oscar Pestorius amekana mashitaka ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao ya Valentine mwaka jana.
Mwendesha mashitaka anasisitiza kuwa Pestorius alimpiga risasi aliyekuwa mpenziwe Reeva baaya ya ugomvi baina yao lakini amejitetea akisema alimpiga risasi kimakosa akidhani mwizi amevamia nyumba yake.
Hukumu ya Pistorius: Jaji aanza kumbana na uzembe wa kutumia silaha
Jaji anasoma mashitaka na tayari anampata na hatia ya kutumia kizembe silaha katika maeneo tofauti, kuhatarisha amani na kuharibu mali.
anaendelea
Jaji:Ushahidi ulitolea na mashahid ni mkanganyiko na hukubaliki. Watazingatia ushahidi wa kiteknologia mfano rekodi za mtitiriko wa matukio na jinsi yalivyorekodiwaatika katika vyombo va mawailiano; simu nk
Jaji: Jaji aatia saka ueteziwa Pistoriu juu ya sabbu ya ufyatua, kulenga mlango na kuojiua kichokuwa nym ya mlango
Suala tete ni ni kama mtuhumiwa alipanga na kutekeleza mauaji ya mpenzi wake.Oscar Pistorius kujua hatma yake
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amewasili mahakamamni kujua uamuzi wa kesi ya mauaji ya mapenzi wake inayomkabili.
Jaji Thokosile Masipa ndiye anatayetoa uamuzi huo.
Pistorius huenda akafungwa jela miaka 25 ikiwa atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake.
Oscar Pestorius amekana mashitaka ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao ya Valentine hapo mwaka jana.
Mwendesha mashitaka anasisitiza kuwa Pestorius alimpiga risasi aliyekuwa mpenziwe Reeva baaya ya ugomvi baina yao lakini amejitetea akisema alimpiga risasi kimakosa akidhani mwizi amevamia nyumba yake.
Gari ya kampuni ya Tashrif yakamatwa Maili moja.
Gari ya kampuni ya Tashrif imezuiliwa (T 517cfy )kwenda Tanga na police trafc baada ya kuonekakana ina tairi viparavipara!!Yaani tairi za nyuma zile za ndani ni vipara lakini za nje ni mpya.Kwa hiyo wameambiwa wabadilishe tairi ndo gari iondoke.Hizi ajali nyingine ni ubahili wa wamiliki wa vyombo vya usafiri
Gari la Mafuta laungua Moto
Gari la mafuta limeteketea lote kwa moto nje kidogo ya mji wa Morogoro kuelekea Dodoma. Ni umbali wa kilomita 15 kutoka Morogoro mjini. Gari hilo ambalo sikuweza kufahamu kwa haraka ni mali ya kampuni gani limeteketea kwa moto na kuziba barabara hali iliyosababisha foleni kubwa sana.
Jeshi la kuzima moto limefika na kutoa msaada kuzima moto tu lakini gari lenyewe hata kichwa hakieleweki. Angalia picha ambazo nimebahatika kupata kwakuwa nami nilikuwa ndani ya basi nikisafiri.
Basi la HOOD T.770 AVL lapata ajali usiku huu Mbeya - Arusha
Basi la Kampuni ya HOOD LTD namba T.770 AVL lilikuwa linatoka Mbeya kuelekea Arusha usiku huu limegongana uso kwa uso na lori katika maeneo ya Kijiji cha Mbwewe,basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Omary Saidi, katika ajali hiyo kondakta wa bus hilo aitwaye kwa jina moja Hamisi amevunjika miguu yote.Wana JF kwa sasa picha hazikuweza kupatikana kutokana na wakazi wa pale kushindwa kupiga picha kutokana na uwezo wa simu zao.
HATARI: Meli yavuja mafuta, athari kubwa kutokea kwa wakazi wa Dar
Wakuu,
Meli hii ina zaidi ya mwaka katika Pwani ya Kunduchi nyuma ya Hoteli ya Kunduchi Beach.
Kwa sasa (ninapoandika) inamwaga mafuta mengi baharini.
Tuesday, September 9, 2014
Mtoto wa Obasanjo ajeruhiwa Nigeria
Wanamgambo wa Boko Haram
Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olesugun Obasanjo amejeruhiwa kwa risasi wakati wa mapambano na wanamgambo wa kiislamu Boko Haram.
Luteni Kanali Adeboye Obasanjo alijeruhiwa siku ya jumatatu wakati jeshi la Nigeria lilipokuwa likipambana kuudhibiti mji wa Michika karibu na mji wa Mubi mji uliokuwa ukidhibitiwa na wanamgambo katika jimbo la Adamawa.
Msemaji wa zamani wa Olusegun Obasanjo ameiambia BBC kuwa kanali Adeboye anaendela vizuri.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao, wanajeshi wameondoka kwenye kambi za kijeshi na chuo katika jimbo hilo kufungwa.
Wanamgambo wa Boko haram wamedhibiti miji mingi kaskazini mashariki na kutangaza kuwa himaya za kiislamu
Ebola inaenea kwa kasi nchini Liberia
Ugonjwa wa Ebola unaenea kwa kasi nchini Liberia huku maelfu ya watu wakiambukizwa upya na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka katika muda wa wiki tatu zijazo.
Hii ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.
Shirika hilo linasema kuwa njia zinazotumika kukabiliana na janga la Ebola hazijafanikisha vita dhidi ya Ebola.
Takriban watu 2,100 wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika kanda ya Afrika Magharibi hasa katika mataifa ya Guinea, Liberia, Sierra Leone na Nigeria mwaka huu.
Kwa mujibu wa shirika hilo wahudumu 79 wa afya pia wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Kadhalika shirika hilo limesema kuwa, mashirika yanayopambana na mlipuko wa ugonjwa huo, yanahitajika kuongeza juhudi.
Wakati huohuo , shirika la madaktari wasio na mipaka la Medecins Sans Frontieres linasema kuwa limelemewa kabisa na idadi inayozidi kuongezeka ya wagonjwa wa Ebola nchini Liberia.
Shirika hilo linasema kuwa kituo chake cha kutoa matibabu mjini Monrovia huwarudisha nyumbani watu wanaohitaji matibabu kila siku .
Msemaji wa shirika hilo Sophie Jane Madden aliambia BBC kuwa hali hiyo sasa ni ya vurugu na isiyodhibitika ambapo ametoa wito wa msaada wa kimataifa.
Mapema shirika la afya duniani WHO lilionya kuwa Liberia huenda ikashuhudia maelfu ya visa vya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ebola majuma yanayokuja.
Watu 1000 tayari wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi.
Kikwete na UKAWA wakubaliana
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TDC) alipokutana nao jana Ikulu ndogo mjini Dodoma. Picha na Ikulu
NA WAANDISHI WETU DAR, DODOMA
HATIMAYE mvutano kati ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Serikali umefikia kikomo baada ya pande mbili hizo kukubaliana na Rais Jakaya Kikwete kuboresha Katiba ya mwaka 1977 na kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani.
Hatima hiyo ilifikiwa jana kwenye kikao kilichofanyika kati ya Rais Kikwete na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kinachoundwa na vyama vyenye wabunge ambavyo ni CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF, TLP, UDP na UPDP inayowakilisha vyama visivyo wa wabunge, kilichofanyika Ikulu ndogo mjini Dodoma.
Mkutano wa awali wa viongozi hao ulifanyika Agosti 31, mwaka huu, katika Ikulu ya Kilimani, mjini Dodoma ambapo walipeana majukumu ya kufanya ili kuangalia namna bora ya kufikia mwafaka.
Katika mkutano wa jana, chanzo cha habari kutoka ndani ya mkutano huo kilieleza kuwa viongozi hao walikubaliana kuwa kutokana na mazingira ya sasa, ni vigumu kupata Katiba mpya ambayo itatumika mwakani.
Kutokana na hali hiyo, viongozi hao walikubaliana kuwa ni vyema vyama hivyo vikakaa na kuangalia mambo muhimu ya kuwekwa kwenye Katiba ya sasa.
“Vyama vinatakiwa vikae na kuangalia ni nini cha kuchukuliwa na kuwekwa kwenye Katiba hii ya sasa, baada ya kumaliza Uchaguzi Mkuu ndiyo sasa turudi kwenye mchakato wa kuandika Katiba mpya,” alisema.
Alisema kuwa baada ya vyama hivyo kukaa na kukubaliana kitu cha kuweka kwenye Katiba inayotumika sasa, watayapeleka mapendekezo hayo serikalini kisha muswada wa marekebisho ya Katiba utapelekwa bungeni.
Kwenye suala la kuahirishwa kwa Bunge, chanzo kingine kilisema kuwa halikuzungumziwa, lakini busara inatarajiwa kutumika zaidi.
Mwenyekiti TCD
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo, alisema kuwa wamekubaliana kindugu.
Waandishi wa habari walipotaka afafanue kauli yake na kama kukubaliana huko kunamaanisha kusitisha Bunge ama Ukawa kurudi bungeni, Cheyo alisema: “Mimi naongea kama mwenyekiti wa vyama vyote, tumekubaliana kindugu, mazungumzo yalienda vizuri na kesho nitatoa taarifa kamili.”
Mwanasheria Mkuu
Agosti 16, mwaka huu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, alizungumzia ugumu wa rais kuvunja Bunge la Katiba na kusema Katiba mpya ikishindwa kupatikana, iliyopo sasa itafanyiwa marekebisho.
Jaji Werema alikuwa akizungumzia hatima ya upatikanaji wa Katiba mpya na mwenendo wa vikao vya kamati za Bunge Maalumu vinavyoendelea sasa Dodoma, ambavyo vimesusiwa na wajumbe wanaounda Ukawa.
Alisema tathmini iliyofanyika ya mwenendo wa vikao hivyo, imeonyesha kuwa theluthi mbili inayohitajika ili kupitisha vifungu vinavyojadiliwa inapatikana, isipokuwa wasiwasi umebaki kwenye kupitisha vifungu hivyo wakati wa vikao vya pamoja vya wabunge wote.
Jaji Werema alisema kwa kutambua hilo, iwapo akidi ya theluthi mbili ya wajumbe haitapatikana wakati wa kupitisha Katiba iliyopendekezwa, baadhi ya vifungu vitakavyopitishwa vitachukuliwa na kupelekwa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kuingizwa kwenye Katiba ya sasa ya mwaka 1977.
“Kwa sasa akidi kwenye kamati inatosha, tukifikia Bunge kuja na Katiba inayopendekezwa na kama hakuna theluthi mbili, tutarudi kwenye Bunge la kawaida (Bunge la Jamhuri ya Muungano) na kukubaliana, yaliyokuwa hayana ubishi tutayaweka na kuyatumia kwenye Katiba ya sasa, likiwamo suala la mgombea binafsi,” alisema Jaji Werema.
Kaburi lafukuliwa, Maiti iliyokufa kwaajali yaibiwa.
Pichani: ni watu wakiwa wameduwaa karibu na eneo la tukio.
Habari nilizozipata hivi punde kutoka Musoma ni kwamba moja ya kaburi alilozikwa mtu aliyepata ajali Musoma wiki iliyopita limefukuliwa na maiti yake imeibwa.
Nitazidi kuwajuza kadri nitakavyozidi pata habari hii kwa kina.
Kivuko kipya (mv dar es salaam) chakamilika kujengwa na kampuni kutoka denmark
Ile ahadi ya Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli ya kununua kivuko kipya kitakachotoa huduma ya usafiri kati ya Jiji la Dar es Salaam na mwambao wa Bahari ya Hindi hadi Bagamoyo imetimia. Taarifa za uhakikia tulizozipata hivi punde ni kuwa kivuko hicho (Mv Dar es Salaam) kilichokuwa kinajengwa na kampuni kutoka Denmark leo kimeshuka majini na tayari kuanza safari ya kuja Dar es Salaam ambapo kinatarajiwa kufika/kutua Dar es Salaam kati ya wiki tatu mpaka nne zijazo.
Kivuko cha MV Dar es Salaam kitakuwa na kasi kuliko kivuko chochote Afrika ya Mashariki na hasa mwambao wa bahari ya Hindi ukiacha Afrika ya Kusini.
Kivuko hiki ni muendelezo wa juhudi za Wizara ya Ujenzi za kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kujenga barabara za New Bagamoyo (Kawawa JCT - Tegeta); ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit Infrastructure - BRT) ikiwemo kuanza ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka awamu ya pili ; ujenzi wa ‘Flyover’ ya TAZARA na UBUNGO ; barabara za pete (DSM Outer Ring Roads); barabara ya Dar es Salaam – Chalinze Expressway; kupanua barabara ya lami sehemu ya Gerezani (KAMATA – Bendera Tatu) kutoka njia mbili za sasa hadi njia nne; kujenga daraja la Kigamboni linalounganisha Kurasini na Kigamboni, daraja hili linatarajiwa kukamilika mwakani mwezi wa sita.
Nyangumi afia pwani ya Mtwara
Mnyama anayeongoza kwa ukubwa duniani i.e samaki aina ya nyangumi amenasa na kufia ktk pwani ya mtwara jana.
Nategemea maliasili na utalii wangefanya chochote kupreserve in museum this rare specie kabisa ulimwenguni kuliko kuendelea kumuacha anaoza pale kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
WAKAZI wa Msangamkuu, Mtwara Mjini mkoani Mtwara na vitongoji vyake, jana walimiminika katika pwani ya Bahari ya Hindi kumshangaa samaki aina ya Nyangumi mwenye urefu wa futi 48 na tani zaidi ya 30.
Mbali na mshangao huo nyangumi huyo alikuwa kivutio kwa waliomwona huku ikielezwa kwamba mara ya mwisho samaki huyo alionekana zaidi ya miaka 25 iliyopita.
Akizungumza na Tanzania Daima, mvuvi wa samaki huyo Saidi Hassani ‘Ngassa’ alisema Septemba 3 akiwa katika shughuli zake alizivuta nyavu na kubaini kuna uzito usio wa kawaida uliosababisha chombo chake kuvutwa na samaki huyo.
“Baada ya kuona anaweza kuniletea shida nilimuacha samaki huyo akiwa kwenye nyavu nilirudi nyumbani kuwaita watu wengine ili wanisaidie kuvuta nyavu… lakini siku ya kwanza na ya pili ilishindikana hadi siku ya tatu tulimvuta mpaka pwani,” alisema Ngassa.
Ofisa Uvivu Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Saidi Abdallah aliwataka wakazi wa Msangamkuu kutomla samaki huyo kwa kuwa ni sumu, badala yake watumie mafuta yake ambayo ni dawa ya misuli.
Monday, September 8, 2014
Wachina wadai samaki wao
Maharamia wa kichina waliokamatwa wakivua samaki kwenye maji ya Tanzania wanadai samaki (samaki wa Magufuli) na meli yao iliyotaifishwa na serikali. Wachina hao wamedai 'chao' kupitia wakili wao aliyekuwa akiwatetea kwenye kesi ya uhujumu iliyokuwa ikiwakabili mahakamani.
Huo ni mwendelezo wa kuboronga kwa serikali ya CCM, kupitia DPP, ambayo iliifuta kesi halali iliyofunguliwa kihalali mahakamani dhidi ya maharamia hao. Hakukuwa na sababu zozote za msingi kufuta kesi hii ya UHUJUMU UCHUMI. Ufutaji wa kesi hii ni moja ya maamuzi mengi ya kitutusa yanayofanywa na serikali ya CCM ambayo adhari zake ni kubwa sana kwa wananchi wa kawaida wasiokuwa na hatia.
Sasa wale samaki tuliokuwa tukiwatafuna na kuwasifia utamu wake wataanza kututokea puani.
Huo ni mwendelezo wa kuboronga kwa serikali ya CCM, kupitia DPP, ambayo iliifuta kesi halali iliyofunguliwa kihalali mahakamani dhidi ya maharamia hao. Hakukuwa na sababu zozote za msingi kufuta kesi hii ya UHUJUMU UCHUMI. Ufutaji wa kesi hii ni moja ya maamuzi mengi ya kitutusa yanayofanywa na serikali ya CCM ambayo adhari zake ni kubwa sana kwa wananchi wa kawaida wasiokuwa na hatia.
Sasa wale samaki tuliokuwa tukiwatafuna na kuwasifia utamu wake wataanza kututokea puani.
Friday, September 5, 2014
mateso dhidi ya mahabusu Tanzania
Watuhumiwa wa ugaidi walio kwenye magereza ya Dar es Salaam wanalalamika kuteswa kikatili na kudhalilishwa kijinsia wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola wakilazimishwa kukiri makosa wanayoshitakiwa.
Safu ya viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho Zanzibar, ambao baadhi yao wamefunguliwa mashitaka ya ugaidi Tanzania Bara.
Katika Mbiu ya Mnyonge, Mohamed Dahman anahoji ni kwa namna gani tuhuma kama hizi zinatolewa na kunyamaziwa kimya na mamlaka husika katika wakati ambapo dunia inazungumzia utawala wa sheria na haki za binaadamu, zikiwemo za wale walio mikononi mwa vyombo vya dola!
Kusikiliza makala nzima, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Marekani yasema imemuua Ahmed Godane
Taarifa kutoka idara ya ulinzi ya Marekani Pentagon zinasema kuwa mmoja wa wanzilishi wa kundi la Al Shabaab Ahmed Godane ameuawa.
Marekani imesema kuwa kuuawa kwa Godane ni hatua kubwa sana katika harakati dhidi ya wapiganaji hao wamekuwa msumari mkali kwa mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na hata kwa serikali ya Somalia yenyewe.
Katibu wa Pentagon Nchini Rear Admiral John Kirby ametangaza kuwa Ahmed Godane ameuawa katika oparesheni iliyofanywa nchini Somalia Jumatatu wiki hii.
Kwa Mujibu wa Admiral Kirby, kuuawa kwa Godane ni pigo kubwa zaidi kwa kundi hilo la Al shabaab na itasaidia kukabiliana na ugaidi unaofanywa na kundi hilo eneo la Afrika Mashariki.
Marekani imekuwa ikishirikiana na washirika wake wakuu kukabili wapiganaji hao wa AL shabaab ambapo katika miaka ya hivi karibuni wamezidisha mashambulio sio tu nchini Somalia bali hadi nchi jirani.
Wiki iliyopita Kikosi cha kulinda amani chini ya mwavuli wa Muungano wa Afrika AMISOM kikishirikiana na majeshi ya serikali ya Somalia kilianzisha oparesheni kali kuwasaka wapiganaji hao wa AL shabaab. Na kufikia mwanzoni mwa wiki hii Marekani ikajiunga katika oparesheni hiyo ambapo walishambulia msafara ambao Ahmed Godane alishukiwa kuwa ndani.
Walioshuhudia waliambia BBC kuwa muda mfupi baada ya msafara huo kushambuliwa, ndege za kivita za helikopta zinazoaminiwa kuwa za Marekani zilishuka na kubeba maiti zote zilizo kuwepo. Kwa hiyo kwa muda hakukuwa na thibitisho lolote iwapo Godane mwenyewe aliuawa au la.
Upande wa AL shabaab nao walianza kukusanya watu katika kijiji karibu na eneo hilo la Shebeele ambako shambulio lilifanywa na kuwaua au kuwateka wengijne ambao hadi sasa hawajulikani waliko.
AL shabaab hawakuzungumzia iwapo Godane alikuwa miongoni mwa waliouawa.
Leo asubuhi kulikuwa na picha zilizo sambazwa katika mtandao ambazo hazikuthibitishwa zilizodai kuwa ni Ahmed Godane bado alikuwa hai.
Al shabaab hawajasema lolote baada ya tangazo la Pentagon kuthibitisha kifo cha Godane
Watu 36 wafariki katika ajali Tanzaniai
Takriban Watu 36 wamefariki na wengine 79 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu, mabasi mawili na gari dogo ajali iliyotokea Mkoani Mara, Kaskazini mwa Tanzania.
Eneo hasa ambako ajali hiyo ilitokea ni katika barabara ya Musoma- Mwanza mabasi hayo yaligongana uso kwa uso katika eneo la Saba Saba wilaya ya Butiama mkoani humo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mara, Alex Karangi ameiambia BBC kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa tano asubuhi katika eneo la sabasaba
Kamanda Karangi amesema Kabla ya kugongana uso kwa uso kwa mabasi hayo , gari dogo liligongwa na basi lililokuwa likitoka mkoani mwanza na kutumbukia mtoni.
Uchunguzi unafanyika kubaini chanzo cha ajali hiyo na hivi sasa majeruhi wako hospitali ya mkoa wilayani Musoma.
Utaratibu wa kuwatambua waliopoteza maisha katika ajali hiyo unaendelea.
Kongamano la katiba la vijana jmosi 6 sept
Kesho jumamosi ktk ukumbi wa blue pearls ubungo plaza kuanzia saa 3 mpaka saa 8 mchana.
Wazungumzaji watakua.
Humphrey Polepole
John john Mnyika
Maria Sarungi
Paul Makonda
Mada: agenda za vijana ktk mchakato wa katiba.
Nitasikitika sana kama itv haitarusha hili kongamano kutokana na ule mkwara wa 6.
Nawasilisha.
Subscribe to:
Posts (Atom)