Gari la Mafuta laungua Moto
Gari la mafuta limeteketea lote kwa moto nje kidogo ya mji wa Morogoro kuelekea Dodoma. Ni umbali wa kilomita 15 kutoka Morogoro mjini. Gari hilo ambalo sikuweza kufahamu kwa haraka ni mali ya kampuni gani limeteketea kwa moto na kuziba barabara hali iliyosababisha foleni kubwa sana. Jeshi la kuzima moto limefika na kutoa msaada kuzima moto tu lakini gari lenyewe hata kichwa hakieleweki. Angalia picha ambazo nimebahatika kupata kwakuwa nami nilikuwa ndani ya basi nikisafiri.
No comments:
Post a Comment