Majambazi toka kenya yaua na kupora fedha kwa mtu mmoja katika eneo la holoholo mkoani Tanga.


Kufuatia makundi ya uhalifu yaliyokuwa na silaha aina ya ''Short Gun'' yanayodaiwa kutoka nchi jirani ya Kenya kuvamia wafanyabiashara kisha kupora mali, fedha na kuua mtu mmoja katika eneo la horohoro lililopo mpakani mwa Kenya na Tanzania, jeshi la polisi mkoani Tanga limeanza operesheni maalum ya kuwasaka baadhi ya watu wanaodaiwa kuwakaribisha wahalifu hao.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga Bwana Freisser Kashai ameiambia ITV kuwa makundi hayo ya uhalifu yalifanya mauaji hayohayo hivi karibuni na inadaiwa kuwa wapo baadhi ya watanzania wanashirikiana nao hivyo amewaomba wananchi waishio katika vijiji vilivyopo jirani na mpaka unaotenganisha nchi zote mbili kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha watu hao wanakamatwa.

Katika tukio jingine jeshi la polisi limekamata shehena ya dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 68 zilzokuwa zimefungwa katika ujazo wa kilo moja kwa kila kifurushi katika eneo la kiomoni lililopo jijini Tanga zikipelekwa kwa mawakala wanaosambaza bidhaa hiyo haramu kisha kumtia mbaroni msambazaji aliyejulikana kwa jina la Ally Ramadhani ambaye ni mkazi wa sahare jijini Tanga. Mia